How can we help?

Sign in

Hesabu ya Alama ya Shughuli

Alama ya shughuli inakupa maelezo ya jumla ya safari uliozofanya kwa siku. Alama ya shughuli kwa siku inahesabiwa kwa kuzingatia safari 40 za mwisho na alama zitaongezeka kwa kila safari mpya inayofanyika.

Kama ukikubali na kukamilisha kila safari, alama yako ya shughuli itakuwa na mabadiliko chanya ili mradi tu uwe hujakataa au kukatisha asilimia 20% au zaidi ya maombi ya safari.

Kama ulikataa  20% ya safari 40 za mwisho, moja kwa moja akaunti yako itazuiliwa na mfumo wetu.

Kuangalia alama yako ya shughuli:

  • Guda kuelekea juu kwenye orodha kuu
  • Gusa kwenye shughuli (Activity)

Kipengele hiki kina sehemu kuu tatu:

  • Sehemu ya masaa inaonyesha jumla ya muda uliosubiri na muda ulioendesha
  • Sehemu ya safari inaonyesha jumla ya safari ulizokamilisha kutoka kwenye maombi yote uliyopata. Unaweza kuchagua muonekako wa uwiano au asilimia kwa kugusa sehemu ya Alama
  • Sehemu ya kukatisha inaonyesha sababu ya kukatisha safari 50 za hivi karibuni na inaonyesha vidokezo kuhusu jinsi ya kuboresha ufanyaji wako wa kazi

Sehemu zote tatu zinaweza kubadilishwa kuonyesha taarifa za wiki ya sasa, iliyopita au miezi mitatu iliyopita. Unaweza kuona pia siku tofauti kwa kugusa kwenye Kisehemu chenye rangi ya bluu

Kumbuka: Kama ukikatisha safari kwa sababu mteja hakutokea baada ya dakika tano za kumsubiri mteja basi Alama yako ya kazi haitaathirika.

Was this article helpful?