How can we help?

Sign in

Boresha Viwango Vyako

Abiria wanaweza kutoa tathmini ya viwango vya uzoefu wa dereva katika uendeshaji kwa kila baada ya safari. Safari 40 za mwisho ziliotolewa tathmini na abiria zitahesabiwa ili kupata alama ya wastani. Na hesabu hiyo itaonekana kwenye kila safari zilizotolewa tathmini.

Vidokezo ili kupata viwango vya juu:

  • Kwa ujumla kuwa mkarimu na mwenye heshima
  • Saidia kufungua buti au mlango wa gari kwa abiria mwenye mizigo
  • Heshimu na fuata sheria za barabarani na jali watumiaji wengine wa barabara
  • Epuka aina yoyote ya mgogoro, kuwa mtulivu na mvumilivu wakati wa changamoto
  • Kila mara muulize abiria kama atapenda kiyoyozi au radio kuwashwa au kuzimwa
  • Kuwa na nyaya za moto kwa simu za Apple na Android
  • Weka gari yako katika hali ya usafi
  • Kuwa na manukato na uyatumie kila baada ya muda fulani
  • Weka jojo au pipi ndani ya gari yako
  • Kuwa na waya wa AUX

Toa huduma yenye ubora wa hali ya juu kwa abiria wako ili kuweka tathmini ya huduma yako katika viwango vya juu!

Was this article helpful?