How can we help?

Sign in

Muongozo kuhusu Safari katikati ya Safari

Ili kutumia muda wa kuendesha na Bolt kwa ufanisi zaidi, dereva anaweza kuthibitisha safari mpya kabla ya kumaliza safari zinazoendelea.

Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

  • Utapokea ombi la safari mpya na litadumu kwa sekunde 20 wakati ukiwa kwenye safari
  • Utakapo thibitisha ombi la safari mpya, utaona makadirio ya muda wa kufika alipo abiria anayeita
  • Wakati safari inaendelea, utaona jina la eneo alipo abiria anayefuata  juu ya skrini

Wazo Kuu:

  • Unaweza kupata maombi ya safari katikati ya safari endapo abiria unayesafiri nae wakati huo ameweka uelekeo
  • Kabla hujathibitisha ombi jipya la safari, inashauriwa kuhakikisha abiria uliyenaye amefikia uelekeo wake
  • Unapokamilisha safari ya sasa unaweza kuendele na eneo alipo mteja anayefuata mara moja
  • Kukataa ombi la safari katikati ya safari kutaathiri alama yako ya shughuli. Kama hutaki kupokea haya maombi unatakiwa Kuzuia maombi ya safari katikati ya safari

Na kipengele cha maombi ya safari katikati ya safari, utapunguza muda wa kusubiri ombi na hali kadhalika utaongeza kipato na ufanisi wako.

Was this article helpful?