How can we help?

Sign in

Pata Safari Kuelekea eneo Ulilochagua

Kama unahitaji abiria pale unapoamua kwenda nyumbani baada ya kuendesha kwa muda mrefu au unataka kupokea maombi ya safari kueleke eneo fulani,  tumia kipengele kiitwacho safari kuelekea eneo ulilochagua.

Jinsi kipengele hiki kinavyofanya kazi:

  • Gusa alama ya kujumlisha (+) kwenye skrini
  • Gusa sehemu ya kuweka eneo
  • Unaweza kuweka nyumbani, au eneo unalopendelea
  • Ili kuondoa kupata safari eneo ulilochagua gusa alama X, pembani ya anuani ya uelekeo wako

Unapochagua chaguo hili utapokea safari zinazoishia karibu na uelekeo uliochagua. Tutaondoa maombi yote ya safari zilizo mbali na njia yako, hivyo muda wa kusubiri ombi unaweza kuwa mrefu kidogo kuliko kawaida.

Hesabu ya fikio

  • Kipengele hiki kina kikomo cha kutumika kwa siku kama ilivyooneshwa kwenye App na kikomo hicho kitategemea na mji
  • Kila siku usiku hesabu ya eneo ulilochagua itajirekebisha na kurudi katika hali yake ya mwanzo
  • Uelekeo ambao haujatumika hautaendelea kuwepo kwa siku inayofuata
  • Safari ambayo imeanza kabla ya saa sita usiku na ikaendelea mpaka siku inayofuata itahesabika kama ni ya siku iliyopita.

Vizuizi

  • Kipengele kitazuia namba ya maombi ya safari unayopokea, kwani utapokea safari zinazofanana au kuelekea kwenye uelekeo uliochagua
  • Tafadhali kumbuka kuwa kuna kampeni ambazo hazikubali safari zenye uelekeo unaofanana

Kumbuka: Kipengele hiki kinapatikana kwenye baadhi ya nchi tu. Hakikisha unatumia tolea jipya la App.

Was this article helpful?