How can we help?

Sign in

Kumpigia Mteja

Iwapo imetokea hali fulani, kwa mfano mteja hakuonekana baada ya dakika 4-5 za kusubiri au aliacha kitu kwenye gari, utahitaji kuwasiliana na mteja.

Kumpigia mteja baada ya kumaliza safari:

  • Nenda kwenye historia ya safari
  • Nenda kwenye safari husika
  • Chagua pigia mteja, chaguo hili litapatikana ndani ya masaa 24 baada ya safari kukamilika

Kumpigia mteja kabla ya safari kuanza:

  • Bonyeza kwenye orodha iliyopo kona ya kulia juu.
  • Bonyeza chaguo la kumpigia abiria

kumbuka:

  • Unaweza kumpigia mteja kwa kutumia nambari ya simu iliyosajiliwa kwenye akaunti yako. Unaweza kubadili nambari ya simu mwenyewe kupitia portal ya dereva
  • Utaweza kuwasiliana na abiria baada ya kukubali ombi na ndani ya masaa 24 baada ya safari kukmilika
  • Baada ya masaa 24, suala au swali lolote litatakiwa kuripotiwa kwa Timu ya msaada kupitia App
  • Kama mteja alikatisha safari, chaguo la kupiga simu litaondolewa na hapatakuwa na njia ya kuwasiliana na mteja.
Was this article helpful?